• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaitaka Marekani ichangie ushirikiano wa kunufaishana kati ya nchi hizo mbili

    (GMT+08:00) 2019-09-16 19:50:30

    China imeitaka Marekani iachane na mtazamo wa Vita Baridi, kuangalia kwa usahihi China na uhusiano kati ya nchi hizo mbili, na kufanya juhudi kubwa katika kuhimiza ushirikiano wa kusaidiana kati yao ili kuwanufaisha wananchi wa nchi hizo mbili na wa dunia.

    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bibi Hua Chunying amesema hayo akizungumzia hotuba aliyotoa msaidizi wa waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Christopher Ford kwamba serikali ya Marekani inapanga hatua za "serikali kamili" za kukabiliana na changamoto za kiusalama zinazotolewa na China kwa Marekani na washirika wake. Bibi Hua amesema China siku zote ni mjenzi wa amani ya dunia, mchangiaji wa maendeleo ya dunia na mlinzi wa utaratibu wa kimataifa, sifa ambazo hazitakiwi kuharibiwa na nchi au mtu yeyote.

    Bibi Hua pia amesema China inapinga ajenda inayobuniwa na watu makusudi ya eti "usalama wa mtandao wa 5G wa Huawei", na kutumia ovyo kisingizio cha "usalama wa taifa" kuzuia kampuni ya China kujiendeleza na kufanya ushirikiano katika sekta ya teknolojia ya habari na mawasiliano.

    Habari nyingine zinasema waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi ataongoza ujumbe kushiriki kwenye mjadala wa kawaida wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa utakaoanza tarehe 24 mwezi huu mjini New York, na pia kushiriki kwenye mkutano wa kilele wa utekelezaji wa mabadiliko ya hali ya hewa ya Umoja huo na mkutano wa kilele wa malengo ya maendeleo endelevu kwa niaba ya rais Xi Jinping.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako