• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waziri Mikuu wa China awasili nchini Russia kwa ziara rasmi

  (GMT+08:00) 2019-09-16 20:45:12

  Waziri Mkuu wa China Bw. Li Keqiang amewasili mjini St. Petersburg kwa ajili ya ziara ya siku tatu nchini Russia.

  Naibu waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Le Yucheng amesema ziara hii inafanyika wakati nchi hizo mbili zinaadhimisha miaka 70 ya uhusiano wa kibalozi na kufungua zama mpya ya ushirikiano kati yao. Wakati wa ziara hiyo, Bw. Li na waziri mkuu wa Russia Dimitry Medvedev wataendesha mkutano wa 24 wa kawaida wa wakuu wa serikali za nchi hizo mbili.

  Bw. Le amesema mkutano huo utafuatilia malengo mawili. Kwanza ni kuhimiza utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa na wakuu wa nchi hizo mbili, kuhimiza mafungamano kwenye maslahi, na kuimarisha msingi wa kimali wa uhusiano wa pande mbili.

  Pili ni kuchangia busara ya nchi hizo mbili na kutoa sauti yao katika kuunga mkono mambo ya pande nyingi, uchumi ulio wazi, kufungua uchumi na kuhimiza biashara na uwekezaji.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako