• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • IGAD na Ethiopia kujenga kituo chenye ubora kabisa cha kupambana na saratani

  (GMT+08:00) 2019-09-17 08:46:59

  Jumuiya ya Maendeleo ya Kiserikali ya Nchi za Afrika Mashariki (IGAD) na serikali ya Ethiopia jana walizindua mpango wa kujenga kituo chenye ubora kabisa cha saratani cha kikanda kitakachogharimu kiasi cha dola za Kimarekani milioni 450, kikiwa na lengo la kuondoa mzigo unaoendelea kukua kwa huduma za afya za saratani.

  Akiongea kwenye hafla ya kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho, Katibu Mtendaji wa IGAD Mahboub Maalim, amezitaka nchi wanachama pamoja na washirika kushirikiana pamoja katika kutambua mipango ya kituo hicho ili kuwapa matumaini wananchi wanaoteseka na saratani katika kanda hiyo.

  Kituo cha Saratani cha Afrika Mashariki, ambacho kinatarajiwa kumalizika ndani ya miaka miwili ijayo, kitashughulikia mahitaji yanayohusiana na huduma za afya ya saratani katika nchi nane wanachama wa IGAD ambazo ni Djibouti, Ethiopia, Eritrea, Kenya, Somalia, Sudan, Afrika Kusini na Uganda.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako