• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya kuzindua mpango wa utafiti wa Afrika ili kuongeza kasi ya kilimo cha kisasa

    (GMT+08:00) 2019-09-17 08:48:01

    Kenya jana ilizindua mpango wa Afrika wa kutoa mafunzo kwa wanasayansi wa kizazi kijacho ambao watasaidia juhudi zinazoendelea za kuongeza kasi ya kilimo cha kisasa katika bara hilo.

    Kituo cha Utafiti wa Kilimo na Maendeleo cha Wanawake nchini Kenya AWARD kikishirikiana na mifuko mbalimbali wamezindua mafunzo ya kwanza kwa wanasayansi wa Afrika ambao watafanya utafiti utakaosaidia kilimo cha kisasa kutokana na hali ya hewa. Wanasayansi watajumuishwa kwenye Mafunzo ya One Planet ambayo ni mpango wa kukuza kazi kwa vijana wa Afrika pamoja na wanasayansi wa Ethiopia wanaotarajiwa kufanya utafiti juu ya uvumbuzi na mafunzo ya vitendo yatakayosaidia kilimo kinachohimili hali ya hewa kwa wakulima wadogo.

    Mpango huo utakaogharimu shilingi bilioni 2 za Kenya utalenga kwenye utafiti wa pamoja, mafunzo na mipango ya kubadilishana yenye madhumuni ya kuwaongezea uwezo wanasayansi wachanga wa Afrika watakaofungamanishwa na wakulima wadogo wanaoendesha kilimo cha kisasa kutokana na hali ya hewa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako