• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa Uingereza akutana na mwenyekiti wa Kamisheni ya Ulaya juu ya Brexit

    (GMT+08:00) 2019-09-17 09:04:56

    Waziri mkuu wa Uingereza Bw. Boris Johnson amekutana na mwenyekiti wa Kamisheni ya Ulaya Bw. Jean-Claude Juncker jana Jumatatu huko Luxembourg, ambapo amesisitiza kuwa nchi yake itajitoa kwenye Umoja wa Ulaya Oktoba 31.

    Akihojiwa na wanahabari wa Uingereza baada ya mkutano huo, Bw. Johnson amesema juhudi zimefanywa kwenye mazungumzo katika kutafuta mpango mbadala wa sera ya awali ya kuhakikisha mpaka wa Ireland unakuwa wazi kama ilivyokuwa sasa baada ya Brexit (Irish backstop), ili kuepusha uwekaji wa mpaka halisi wa kuzuia watu na mizigo kusafiri kwa uhuru katika kisiwa cha Ireland.

    Bw. Johnson amesema sasa wamefikia hatua ambayo wanahitaji kuanza kuharakisha kazi kama ilivyokubaliwa kati yake na Jean-Claude Juncker na mjumbe wa Umoja wa Ulaya kwenye mazungumzo ya Brexit Michel Barnier.

    Ameongeza kuwa atafuata katiba na sheria lakini Uingereza lazima ijitoe Umoja wa Ulaya Oktoba 31, na hakuna uwezekano wa kuahirisha ratiba hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako