• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Shirika la IAEA laanza mkutano mkuu wakati hali ya Iran ikizidi kuwa na wasiwasi

  (GMT+08:00) 2019-09-17 09:11:34

  Mkutano mkuu wa 63 wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Kimataifa IAEA umefunguliwa huko Vienna, kufuatia kuongezeka kwa hali ya wasiwasi katika makubaliano ya nyuklia ya Iran.

  Wengi kati ya nchi wanachama 171 wa shirika hilo wanahudhuria mkutano huo ulioanza jana Jumatatu na kuendelea hadi Ijumaa. Ajenda za mkutano huo ni pamoja na kuhakikisha usalama na usimamizi wa Shirika la IAEA katika Mashariki ya Kati, Korea Kaskazini pamoja na masuala yanayohusiana na usalama wa mionzi na njia za kuimarisha shughuli za ushirikiano wa kiufundi za shirika hilo.

  Akizungumzia mgogoro kuhusu makubaliano ya nyuklia ya Iran, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa shirika la IAEA Bw. Cornel Feruta amesema wiki iliyopita, alifanya mazungumzo na maofisa waandamizi wa Iran, na kuendelea kusisitiza umuhimu wa ushirikiano wa pande zote wa Iran katika utekelezaji wa makubaliano ya kuhakikisha usalama na itifaki za ziada.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako