• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • KUOGELEA: Uganda yanyakua medali ya dhahabu kupitia kwa kinda wake

  (GMT+08:00) 2019-09-17 09:29:24

  Muogeleaji wa Uganda Kirabo Namutebi mwenye umri wa miaka 14 amewatoa kimasomaso Uganda baada ya kushinda medali ya dhahabu katika michuano ya ubingwa wa kuogelea wa Afrika inayoendelea nchini Tunisia.

  Namutebi ameshinda katika mita 50 freestyle akitumia dakika 27:33 na aina ya Breaststroke akitumia dakika 35:13. Akizungumza mara baada ya ushindi huo, Namutebi amesema anajisikia fahari kupeperusha vyema bendera ya taifa lake la Uganda.

  Naye rais wa shirikisho la kuogelea la Uganda, Dkt. Donald Rukare amesema, medali iliyobebwa na muogeleaji huyo ni ishara tosha kuwa Uganda inaweza, na kuwataka wazazi kuwaruhusu na kuendeleza vipaji vya watoto wao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako