• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Kocha wa Yanga awatoa hofu mashabiki, aamini wataitoa ZESCO

  (GMT+08:00) 2019-09-17 09:29:43

  Kocha wa Yanga ya Tanzania, Mwinyi Zahera raia wa DRC amewasisitiza mashabiki wa timu hiyo kutembea kifua mbele wala wasitishwe na sare ya ya bao 1-1 dhidi ya Zesco kwenye Uwanja wa Taifa.

  Yanga ililazimishwa sare hiyo kwenye mechi ya kwanza ya raundi ya kwanza ya ligi ya mabingwa Afrika huku timu hizo zikirudiana Septemba 27 ugenini mjini Ndola Zambia. Bao la Yanga lilifungwa na Patrick Sibomana dakika ya 25 kwa mkwaju wa penati huku lile la Zesco likipachikwa na Thabaan Kamusoko kwa shuti kali la nje kidogo ya 18 dakika za nyongeza.

  Licha ya mashabiki wa Yanga kuonekana kunyongea kutokana na bao la usiku pamoja na kejeli za wenzao wa Simba ambao walikuwa wakiishangilia Zesco, Zahera amesisitiza kwamba; Kutoka na sare hiyo haimaanishi kwamba wameyaaga mashindano, wanauwezo wa kushinda bao 1 ugenini kama tulivyofanya kwa Township Rollers.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako