• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RIADHA: Koech na Chepchirchir waendele kuipatia Kenya sifa Sanlam Cape Town Marathon

    (GMT+08:00) 2019-09-17 09:30:16

    Kenya imeendelea kufanya vizuri katika riadha kupitia wanariadha wake, ambapo safari hii imepata medali ya mbio za kilomita 42 za Sanlam Cape Town kupitia Edwin Kibet Koech na Celestine Chepchirchir nchini nchini Afrika Kusini.

    Koech ametumia saa 2:09:20 kukamilisha umbali huo na kuwa mwanamume wa kwanza kutoka Kenya kunyakua taji hili baada ya Shadrack Kemboi mwaka 2015.

    Naye mwanadada Chepchirchir pia amekuwa Mkenya wa kwanza kushinda kitengo cha wanawake tangu Isabella Ochichi aibuke mshindi mwaka 2015.

    Koech alimaliza kitengo chake sekunde 0.05 mbele ya Mkenya mwenzake Daniel Muindi (2:09:25) nao Mohamed Ziani (Morocco), Elroy Galant (Afrika Kusini) na Joseph Khoarahlane (Lesotho) wakafunga mduara wa tano bora.

    Chepchirchir alikata utepe kwa kutumia saa 2:26:44na kufuatwa kwa karibu na Waethiopia Nurit Shimels aliyetumia saa 2:27:40 na Gete Tilahun amemaliza kwa saa 2:28:32. Mashindano hayo ya 13 yameshirikisha wanariadha zaidi ya 7,000.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako