• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Magwiji wa Afrika waanza vyema ligi ya mabingwa Afrika

  (GMT+08:00) 2019-09-17 09:30:32

  Wakati vigogo wa soka barani Afrika wakianza vizuri mechi zao za kwanza za raundi ya kwanza ya ligi ya mabingwa Afrika, timu kutoka ukanda wa Afrika Mashariki zimejiweka katika nafasi ngumu ya kuingia hatua ya makundi.

  Mabingwa watetezi Esperance kutoka Tunisia wameanza kampeni ya kutaka kuwa kalbu ya kwanza Afrika kutwaa kombe hilo mara tatu mfululizo kutokana na sare ya bao 1-1 ugenini dhidi ya Elect-Spoti ya Chad.

  TP Mazembe pia walilazimishwa sare ya bila kufungana na wenyeji wao Fosa Juniors ya Madagascar, huku Enyimba nayo walitoka sare na El Hilal ya Sudan.

  Vigogo Al Ahly ya Misri wamenza vizuri kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Cano Spoti ya Equatorial Guinea, nao Raja Casablanca wakiibuka na uhsindi mnono wa magoli 3-1 dhidi ya Al Nasr ya Libya, nao Zamalek wakipokea kichapo cha 2-1 mbele ya wenyeji wao Generation foot ya Senegal mjini Thies.

  Ukanda wa Afrika Mashariki, Gor Mahia imekubali kipigo cha 4-1 ugenini toka kwa USM Alger ya Algeria, nao KCC ya Uganda ikilazimisha sare ya bila kufungana na Petro Atletico ya Angola, Yanga ya Tanzania ikikubali sare ya 1-1 na Zesco ya Zambia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako