• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Msimamo wa ligi ya Uingereza hadi kufikia jana Septemba 16, baada ya Aston Villa kutoka sare na West Ham.

  (GMT+08:00) 2019-09-17 09:30:51

  Jana kulipigwa mechi moja kati ya Aston Villa dhidi ya West Ham United, na matokeo ni kwamba, timu zote zimetoshana nguvu ya kutoka sare pacha.

  Msimamo wa ligi ya Uingereza (EPL) hadi kufikia jana ni kuwa, Majogoo wa Anfield Liverpool wanaongoza ligi hiyo kwa kucheza mechi 5 hadi sasa, wanamagoli 11 ya kufunga na wamekamata alama 15 katika msimamo huo, huku nafasi ya pili ikikaliwa na Manchester City wakiwa wamekwishacheza mechi 5, magoli 10 ya kufunga na alama 10. Tottenham Hotspurs wao wanakamata nafasi ya tatu wakiwa wamecheza michezo 5, wanamagoli 5 ya kufunga na wana alama 8. Huku Mashetani wekundu Mancheseter United wako katika nafasi ya nne, wakiwa wamshacheza michezo 5, wamejipatia magoli 4 na kuwa na alama 8. Leicester City wao wako katika nafasi ya tano, na nafasi ya sita inashikiliwa na watoto wa daraja la Stamford, Chelsea, huku washika bunduki wa jiji la London Arsenal wanakamata nafasi ya saba. Newcastle, Wolverhampton na Watford wenyewe wanakamata mkia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako