• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mahakama kuu ya Uingereza yasikiliza mapingamizi dhidi ya Waziri Mkuu kuhusu kusimamisha bunge

  (GMT+08:00) 2019-09-17 19:33:46

  Mahakama kuu ya Uingereza imeanza kusikiliza mapingamizi dhidi ya waziri mkuu wa Uingereza Bw. Boris Johnson kufuatia uamuzi wake wa kusimamisha bunge kwa muda wa wiki tano, jambo ambalo halijawahi kutokea katika historia ya Uingereza. Mapingamizi haya mawili tofauti yaliyotolewa England na Scotland.

  Wakati usikilizaji unaaza waandamanaji 40 walikuwa nje ya mahakama wakiwa na mabango yenye maneno "linda demokrasia", "fungua tena bunge", "wamemdanganya Malkia". Usikilizaji wa mapingamizi hayo utafanyika kwa muda wa siku tatu, na jumla ya majaji 11 wataamua kama uamuzi wa Bw. Johnson kusimamisha bunge ni haramu.

  Bw. Johnson analaumiwa kwa kumdanganya Malkia na kutumia madaraka yake kwa malengo mabaya. Lakini yeye amekana laumu hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako