• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Umoja wa Afrika watoa mwito wa kuwepo ubunifu katika mapambano dhidi ya kundi la Al-Shabaab nchini Somalia

  (GMT+08:00) 2019-09-17 19:34:11

  Tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) imevitaka vikosi vya Djibouti na Ethiopia kuwa wabunifu zaidi ili kuhimiza mapambano dhidi ya kundi la Al-Shabaab nchini Somalia.

  Naibu Kamanda anayeshughulikia operesheni na mipango wa AMISOM, ambaye amekuwa akitembelea vikosi nchini Somalia kufanya ukaguzi, amevitaka vikosi vya AMISOM kulisaidia jeshi la Somalia kulinda nchi yao na kuidhibiti.

  Mwito umetolewa wakati mashambulizi yanayofanywa na kundi la Al-Shabaab nchini Somalia yanaendelea kutokea. Mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika Bw. Moussa Mahamat amelaani shambulizi lililofanywa hivi karibuni dhidi ya wanajeshi wa Burundi wa AMISOM katika jimbo la Shabelle ya kati.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako