• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Serikali ya mkoa wa utawala maalum ya Hong Kong yatarajia kufanya duru ya kwanza ya mazungumzo na jamii

  (GMT+08:00) 2019-09-17 19:38:03

  Mkuu wa mkoa wa utawala maalumu wa Hong Kong (HKSAR) Bibi Carrie Lam, amesema serikali ya HKSAR itaanza duru ya kwanza ya mazungumzo na jamii wiki ijayo ili kusimamisha vurugu zilizopo na kurudisha utekelezaji wa sheria mkoani humo.

  Bibi Lam amesisitiza mfumo huo wa kufanya mazungumzo si wa mara moja tu, na unatarajia kuwa endelevu na wa muda mrefu. Amesema mazungumzo hayo yatafanyika kwa uwazi, na serikali iko tayari kuzungumzia mada tofauti.

  Bibi Lam anatarajia watu kutoka sekta mbalimbali washiriki na kubadilishana maoni kwenye mazungumzo hayo, na ana imani kuwa mazungumzo ni njia nzuri zaidi kuliko mapambano.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako