• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yasifu uamuzi wa serikali ya visiwa vya Solomon kukubali kanuni ya kuwepo kwa China moja

  (GMT+08:00) 2019-09-17 19:44:30

  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying amesema China inasifu uamuzi wa serikali ya visiwa vya Solomon wa kukubali kanuni ya kuwepo kwa China moja tu, kumaliza uhusiano wa kidiplomasia na Taiwan na kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na China.

  Bibi Hua Chunying amesema China inaunga mkono uamuzi huo muhimu wa visiwa vya Solomon na inapenda kushirikiana na visiwa vya Solomon na kuanzisha kipindi kipya cha maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

  Bibi Hua Chungying amesema kuna China moja tu duniani, serikali ya Jamhuri ya Watu wa China ni serikali pekee halali inayoiwakilisha China, mkoa wa Taiwan ni sehemu isiyoweza kutengwa kutoka China. Huu ni ukweli wa kimsingi na pia ni maafikiano ya jumuiya ya kimataifa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako