• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya kutaifisha shirika la ndege ili kuongeza nguvu yake ya ushindani

  (GMT+08:00) 2019-09-17 19:44:47

  Serikali ya Kenya inapanga kutaifisha shirika la ndege la Kenya mwishoni mwa mwaka huu ili kuongeza nguvu yake ya ushindani.

  Ofisa mkuu mtendaji wa shirika la ndege la Kenya Bw. Sebastian Mikosz amesema mjini Nairobi kuwa washindani wote wa Shirika hilo wanamilikiwa na serikali zao, kwa hiyo wanakuwa na nafuu ya kifedha.

  Amesema serikali imeunda kamati ya kuongoza kazi ya utaifishaji wa shirika hilo kabla ya mwisho wa mwaka huu, baada ya bunge la Kenya kupiga kura kutaifisha shirika hilo.

  Bw. Mikosz amesema mabadiliko ya kisheria yanatakiwa kuwepo, ili serikali inunue hisa za wenye hisa wachache wa shirika hilo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako