• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwafrika wa kwanza kuwa mkuu wa shirika la ISO

    (GMT+08:00) 2019-09-17 19:54:49

    Kwa mara ya kwanza kwa muda wa miaka 70, Mwafrika atakuwa mkuu wa Shirika la Viwango vya Ubora vya Kimataifa (ISO).

    Bw Eddy Njoroge, ambaye pia ni mwanakamati wa Shirika la Viwango vya Ubora Nchini (Kebs) na mwenyekiti wa zamani wa Nairobi Securities Exchange, anatarajiwa kuthibitishwa kama Rais wa kwanza Mwafrika katika Mkutano wa Baraza Kuu la ISO ambalo limeanza mjini Capetown, Afrika Kusini.

    Bw Njoroge aliweka historia kwa kuifanya kampuni ya Kenya Electricity Generation Company (KenGen) kuwa kampuni ya kwanza ya umma kufikia kiwango cha ISO 9001 mnamo mwaka 2004.

    Viwango vya ISO husaidia katika kupenya katika soko la kimataifa na hufafanua viwango ambavyo huduma na bidhaa zinafaa kufuatilia na kufikia ili kusafirishwa nchi zingine.

    Wakati wa uongozi wake, Bw Njoroge atafanya kazi jijini Nairobi ambapo anachukua nafasi ya Bw John Walter wa kutoka Canada.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako