• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uvumbuzi waleta injini mpya kwa maendeleo ya uchumi wa China

    (GMT+08:00) 2019-09-17 20:02:07

    Benki ya Dunia, kituo cha utafiti wa maendeleo cha baraza la serikali la China na wizara ya fedha ya China leo wametoa ripoti ya pamoja ya "China yenye uvumbuzi, injini mpya ya maendeleo ya uchumi wa China", ikionesha kuwa uchumi wa China unabadilika na kuingia katika hali mpya ya kawaida, na uchumi mpya unaibuka kwa haraka kufuatia ongezeko la uwezo wa uvumbuzi. Radio China Kimataifa imetoa tahariri kuhusu ripoti hiyo.

    Tahariri hiyo inasema, hivi sasa uchumi wa China unabadilika kuendelea kwa sifa zaidi kutoka kuendelea kwa kasi zaidi, na injini mpya ya maendeleo ya uchumi wa China imeibuka. Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na idara kuu ya takwimu ya China, mwaka jana alama ya injini mpya ya maendeleo ya uchumi wa China ilifikia 270.3, na kuongezeka kwa asilimia 28.7 ikilinganishwa na mwaka 2017.

    Tahariri hiyo inasema ongezeko la injini mpya ya maendeleo ya uchumi linatokana kwamba, serikali ya China imeendeleza uchumi kwa kuhimiza uvumbuzi, na kutoa sera ya kuunga mkono makampuni kufanya uvumbuzi na kuongeza utafiti wa teknolojia mpya.

    Tahariri hiyo imesisitiza kuwa ili kukabiliana na changamoto ya vitendo vya upande mmoja na kujilinda kibiashara, China itaimarisha nia yake ya kuendeleza injini mpya ya uchumi, na kusukuma mbele mkakati wa kuhimiza maendeleo kupitia uvumbuzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako