• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uganda: Wauzaji mchele Uganda walalamikia ushindani usiokuwa na usawa

  (GMT+08:00) 2019-09-17 20:02:50

  Wauzaji wa mchele nchini Uganda chini ya Chama chao kinachojumuisha wakulima, wazalishaji na wasindikaji wameliomba Bunge iwalinde dhidi ya waagizaji wa mpunga ambao unaingia nchini bila ushuru.

  Akizungumza baada ya kukabidhi ombi kwa Spika wa Bunge Rebecca Kadaga, Bwana Isaac Kashaija, mwenyekiti wa Chama cha Sekta ya Biashara ya Mchele, alisema takriban kampuni 14, zinaangiza mchele bila kulipia ushuru.

  Alisema uagizaji huo unaathiri biashara zao kwani wanalazimika kulipa ushuru wa asilimia 14 na hivyo kupata ushindani usiokuwa na usawa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako