• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mabalozi wa nchi za Afrika wapongeza Xinjiang katika juhudi za kuondoa ugaidi na kuhimiza masikilizano ya kijamii

  (GMT+08:00) 2019-09-17 20:04:57

  Kwa mujibu wa mwaliko wa serikali ya mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uyghur, mabalozi wa nchi 16 za Afrika na Umoja wa Afrika nchini China wametembelea sehemu mbalimbali mkoani humo, ikiwemo kituo cha elimu na mafunzo ya ufundi stadi na msikiti, wakiipongeza Xinjiang kwa kupata mafanikio katika juhudi za kuhimiza masikilizano ya kijamii, kulinda uhuru wa kuabudu, kueneza utamaduni wa jadi wa kikabila, kupambana na ugaidi na kuondoa msimamo mkali.

  Mwakilishi wa Umoja wa Afrika nchini China Bw. Rahmat Allah Osman amesema amefurahia kuona watu wa makabila mbalimbali wakiishi maisha mazuri kwa masikilizano, na amepongeza juhudi zinazofanywa na serikali ya China katika kuhimiza anuwai ya tamaduni na makabila.

  Balozi wa Rwanda nchini China Bw. Martin Mbazutima amesema amejisikia hatua mbalimbali zinazofanywa na serikali ya Xinjiang katika kuhimiza masikilizano kati ya watu wa makabila tofauti na shughuli za kitamaduni.

  Baada ya kutembelea kituo cha elimu na mafunzo ya ufundi stadi mjini Turpan, balozi wa Uganda nchini China Bw. Chrispus Kyonga amesema Xinjiang imechukua hatua nyingi zenye ufanisi katika kupambana na ugaidi, ikiwemo kuwaelekeza vijana kwenye njia sahihi kwa kuwapatia elimu na mafunzo. Ameongeza kuwa Uganda na nchi nyingine za Afrika zinachukia ugaidi na zinapenda kujifunza uzoefu mzuri wa Xinjiang na kushirikiana na China katika vita dhidi ya ugaidi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako