• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kushambuliwa kwa vitu vya mafuta saudia kwapandisha bei

  (GMT+08:00) 2019-09-17 20:11:03

  Gharama ya mafuta imepanda kwa kiwango cha juu kuwahi kushuhudiwa katika miezi minne baada ya mashambulio mawili dhidi ya vituo vya mafuta Saudi Arabia Jumamosi yaliosababisha kumwagika kwa 5% ya mafuta duniani.

  Kiwango cha mafuta ghafi yalipanda kwa 19% kwa thamani ya $71.95 kila mtungi.

  Bei zilishuka kidogo baada ya rais wa Marekani Donald Trump kuagiza kufunguliwa kwa akiba nchini Marekani.

  Huenda ikachukua wiki kadhaa kabla ya vituo hivyo Saudia kurudi katika hali ya kawaida.

  Kampuni kubwa ya mafuta Saudia Aramco imesema mashambulio hayo yalikatiza usambazaji kwa mitungi milioni 5.7 kwa siku.

  Mashambulio hayo dhidi ya vinu katika shina la viwanda vya mafuta saudia vinajumuisha kituo kikubwa duniani cha usafishaji mafuta.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako