• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rwanda: Kagame akutana na wafanyabiashara wa kikanda

  (GMT+08:00) 2019-09-17 20:13:41

  Rais Paul Kagame wa Rwanda ameandaa mkutano na wajumbe wa Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (EABC).

  Wakati wa mkutano, wawakilishi wa jamii ya wafanyabiashara walielezea changamoto ambazo bado zinatatiza biashara na ujumuishaji.

  Mwenyekiti wa baraza hilo Nicholas Nesbitt, alisema kati ya maswala ambayo walijadili ni pamoja na vizuizi visivyo vya ushuru na gharama kubwa ya kusafirisha shehena ya ndege.

  Baraza hilo ni shirika la mwavuli wa waendeshaji wa sekta binafsi katika kanda ya Afrika Mashariki.

  Wafanyabiashara hao pia walimwalika Rais Kagame katika mkutano wa kilele wa biashara utakaofanyika pembeni mwa ule wa Wakuu wa Nchi unaopangwa kufanyika Novemba mwaka huu nchini Tanzania.

  Rais Kagame pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako