• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania, Kenya na Msumbiji zaanzisha mradi wa ukusanyaji takwimu za samaki

    (GMT+08:00) 2019-09-17 20:14:07

    Serikali ya Tanzania, Kenya na Msumbiji wameanzisha mradi wa ukusanyaji takwimu za samaki kwa kutumia teknolojia ili kulinda rasimali hiyo

    Nchi tatu za ukanda wa Magharibi wa Bahari ya Hindi Tanzania, Kenya na Msumbiji zimeanzisha Mradi wa Ukusanyaji Takwimu za Samaki kwa Ukanda wa Afrika Mashariki (Fidea) ili kuwa na taarifa za pamoja zitakazosaidia kulinda na kujua hali ya viumbe hao.

    Katika kikao cha pamoja cha kujadili mradi huo, wadau kutoka nchi wanachama wameshiriki kutoa maoni yao kuhusu mradi huo unaofadhiliwa na nchi ya Ujerumani.

    Mtendaji mkuu Wakala wa Elimu wa Mafunzo ya Uvuvi, Yahya Mgawe amesema takwimu hizo zitakusanywa kwa njia ya kiteknolojia katika timu ya wasimamizi wa nchi zote tatu.

    Amesema takwimu zitachakatwa na kupata habari zitakazosaidia kufanya uvuvi endelevu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako