• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mawaziri wakuu wa China na Russia wakutana na waandishi wa habari

  (GMT+08:00) 2019-09-18 08:41:52

  Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang na mwenzake wa Russia Dimitri Medvedev jana huko Saint-Petersburg walikutana na waandishi wa habari.

  Mawaziri hao wamepongeza matokeo yaliyofikiwa kwenye mkutano wa 24 kati yao. Bw. Li Keqiang amesema, mwaka huu inatimia miaka 70 tangu nchi hizo mbili zianzishe uhusiano wa kibalozi, ambapo maendeleo ya uhusiano huo yanaendana na maslahi ya pamoja ya pande hizo mbili, pia yanasaidia maendeleo ya ustaarabu wa binadamu. Ameeleza kuwa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili umepata mafanikio mapya katika sekta ya nishati na sekta nyingine za jadi, pia umeibuka katika sekta mpya za biashara ya kielekitroniki, uvumbuzi wa sayansi na teknolojia. Pia anatumai kuwa pande mbili zitajadili namna ya kuzidisha ushirikiano, kuongeza thamani ya ziada kwenye ushirikiano wa nishati, na kutimiza lengo la kuongeza maradufu thamani ya biashara kati ya pande hizo mbili kwa wakati uliopangwa.

  Naye Bw. Medvedev amesema, Russia inapenda kushirikiana na China kupanua sekta zinazopewa kipaumbele kutoka sekta ya nishati na kuwa sayansi na tenknolojia ya juu, kutia nguvu mpya kwenye uhusiano wa kiwenzi na ushirikiano wa kimkakati kati ya China na Russia katika zama mpya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako