• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • NDONDI: Fury akiona cha mtema kuni, achakazwa na kukimbizwa hospitali baada ya kujeruhiwa ulingoni

  (GMT+08:00) 2019-09-18 09:04:21

  Bondia Muingereza Tyson Fury amekiona cha mtema kuni na kukimbizwa hospitali baada ya kujeruhiwa kwa kuchakazwa kwa ngumi kali na mpinzani wake, Mswidishi Otto Wallin katika pambano la uzito wa juu kwenye ukumbi wa T-Mobile Arena mjini Las Vegas, Marekani.

  Hata hivyo, Fury alishinda kwa pointi pambano hilo la raundi 10 na kuendeleza rekodi yake ya kushinda mapambano yake yote 30 ingawa baada ya mchezo huo alikimbizwa hospitali kwa matibabu na kushindwa kuzungumza na Waandishi wa Habari.

  Fury anatarajiwa kurejea ulingoni Februari 22 mwakani kwa pambano la marudiano na Deontay Wilder hapo hapo Las Vegas.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako