• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Nembo ya mashindano ya Olimpiki na Paraolimpiki jijini Beijing 2022

  (GMT+08:00) 2019-09-18 09:04:35

  Nembo ya mnyama aina ya Panda mkubwa iliyopewa jina la "Bing Dwen Dwen" na nyingine inayoitwa "Shuey Rhon Rhon" zimezinduliwa jana kwa ajili ya mashindano ya Olimpiki ya msimu wa baridi na michezo ya wenye ulemavu inayotarajiwa kufanyika hapa jijini Beijing China mwaka 2022.

  Nembo hizo zimezinduliwa kwenye uwanja wa mchezo wa magongo wa barafu wa Shougang.

  Rais wa mashindano hayo ya Beijing Chen Jining ameeleza kuwa, nembo mbili zilizozinduliwa kwa ajili ya mashindano hayo zinaelezea utamaduni wa asili wa wachina na utamaduni mpya wa kigeni na kueleza umuhimu wa michezo ya kwenye barafu wakati wa msimu wa baridi.

  Naye rais wa kamati ya Olimpiki duniani (IOC) Thomas Bach alihuduhuria uzinduzi wa nembo hizo na kufurahishwa na hatua kubwa iliyopigwa ya maandalizi ya mashindano hayo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako