• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Ligi ya mabingwa Ulaya- nyasi ziliwaka moto usiku wa jana, Samatta aandika historia

  (GMT+08:00) 2019-09-18 09:04:54

  Hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Ulaya kwa msimu wa 2019/2020 imeanza jana kwa mechi kadhaa kabla ya mchakamchaka mwingine kuendelea leo Jumatano.

  Matokeo ya michezo ya jana, Napoli imewaonyesha mabingwa watetezi Liverpool kuwa soka si tu uzoefu, kwa kuichabanga goli 2-0, huku mashabiki wengi wakishangaa kilichoikumba KRC Genk anayochezea nahodha wa timu taifa ya Tanzania Mbwana Samatta kwa kupokea kipigo cha kuchakaza cha bao 6-2 toka kwa RB Salzburg. Samatta alifunga goli la pili dakika ya 52 ya mchezo.

  Kundi E, Inter Milan imetoka sare ya 1-1 dhidi ya Slavia Prague, huku Borussia Dortmund nayo ikikabwa koo kwa sare ya 0-0 na Barcelona. Kundi G, Lyon wametshana nguvu ya sare ya 1-1 na Zenit St. Petersburg huku Rasenballsport ikiifunga Benfica 2-1. Na mechi za mwisho ni za kundi H, Ajax imeizamisha Lille kwa bao 3-0 na Chelsea imekubali kipigo cha 1-0 toka kwa Valencia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako