• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Mashabiki wa Gor Mahia watoa ya moyoni, wasema Gor Mahia kuitoa USM Alger ni muujiza

  (GMT+08:00) 2019-09-18 09:05:10

  Kipigo cha paka mwizi ilichokipata Gor Mahia ya Kenya cha mabao 4-1 toka kwa wenyeji wao USM Alger ya Algeria katika mechi ya Klabu Bingwa Afrika (CAF), duru ya kwanza ya raundi ya kwanza mnamo Jumapili usiku, kimegawa mashabiki wake.

  Baadhi ya mashabiki hao wanaofahamika kwa jina la utani kama Green Army, wanaamini bado Gor Mahia ina matumaini ya kulipiza kisasi katika mechi ya marudiano jijini Nairobi hapo Septemba 29. Ikiwapiga Waalgeria hao kwa mabao 3-0, itaingia katika mechi za makundi za Klabu Bingwa.

  Vijana hao wa kocha Steven Pollack wasipopata ushindi huo mkubwa jijini Nairobi, basi watateremka katika mashindano ya ambayo ni Kombe la shirikisho.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako