• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • RIADHA: Kamworor azidi kuzoa zawadi baada ya kuvunja rekodi

  (GMT+08:00) 2019-09-18 09:05:24

  Bingwa mara tatu wa riadha za nusu-marathon duniani, Geoffrey Kamworor sasa anakamata rekodi mpya ya dunia ya mbio za kilomita 21 baada ya kutwaa taji la Copenhagen Half Marathon kwa dakika 58:01 nchini Denmark.

  Kamworor, aliyetumia mbio za Copenhagen kujiandaa kurejesha taji la mbio za kilomita 42 za New York, zitakazofanyika nchini Marekani Novemba 3.

  Mbali na kuvunja rekodi ya dunia, muda wa Kamworor pia ulifuta rekodi ya Copenhagen Half Marathon ya dakika 58:40 iliyowekwa na Mbahraini Abraham Cheroben, ambaye ni mzawa wa Kenya, mwaka 2017.

  Kwa upande wa wanawake raia wa Ethiopia, Birhane Dibaba ameshinda mbio hizo kwa saa 1:05:57 akifuatiwa na Wakenya Evaline Chirchir aliyetumia saa 1:06:22 huku Dorcas Tuitoek akitumia saa 1:06:36.

  Kamworor alifuatwa kwa karibu na Mkenya mwenzake Benard Kipkorir Ng'eno alyetumia dakika 59:16, huku Muethiopia Berehanu Tsegu akikamilisha kwa dakika 59:22.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako