• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wataalamu waitaka Afrika Kusini kutatua chanzo cha mashambulizi dhidi ya wageni

  (GMT+08:00) 2019-09-18 09:18:27

  Wataalamu mbalimbali wamesema Afrika Kusini inapaswa kushirikiana na wenzao wa Afrika kutatua chanzo cha mashambulizi yanayotokana na chuki dhidi ya wageni.

  Akiongea na Shirika la Habari la China, Xinhua, mchambuzi wa masuala ya kisiasa katika Chuo Kikuu cha Afrika Kusini Somadoda Fikeni, amesema suala la uhaba wa rasilimali kwenye jamii masikini haliwezi kupuuzwa na serikali zinapaswa kuwa makini juu ya kufuatilia kwa undani jambo hili. Amesema kama chanzo hakitatatuliwa ana uhakika kuwa yatatokea mashambulizi mengine. Tangu mwaka 2008 Afrika Kusini imekuwa ikikabiliwa na mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya wageni ambayo yamesababisha vifo vya watu 70.

  Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Kiuchumi la Msumbuji Eduardo Sango, ameitaka Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC kuingilia kati na kubeba jukumu lake la kulinda uhuru wa watu wa kusafiri pamoja na kusafirisha bidhaa zao barani Afrika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako