• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Taasisi ya Afya ya Sudan Kusini yawapongeza madaktari wa China kwa kutoa huduma bure za kujenga uwezo

  (GMT+08:00) 2019-09-18 09:18:49

  Taasisi ya Afya ya Mafunzo ya Sayansi nchini Sudan Kusini imekipongeza kikundi cha madaktari wa China waliopo nchini humo kwa kutoa huduma bure za kuwajengea uwezo mamia ya wanafunzi wanaosoma afya katika mwaka mmoja uliopita.

  Mkuu wa taasisi hiyo Charles Abe Buli amesema chuo hicho kimeingia kwenye makubaliano ya ushirikiano na timu ya matibabu ya China mwaka jana, ambayo yanawaruhusu wahudumu wa afya wa China kuhadhiri kwa wiki mara mbili katika masomo yanayohusiana na nusu kaputi na ustadi wa kimatibabu. Amesema ni manufaa makubwa kwao kwani kuna baadhi ya vitengo ambavyo vinakosa mihadhara. Hivyo uwepo wa Wachina unaziba pengo na kuboresha masomo.

  Tangu 2013, timu ya matibabu ya China imekuwa ikitoa huduma bure za matibabu nchini Sudan Kusini na pia kusaidia kuwajengea uwezo wafanyakazi na wanafunzi wa afya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako