• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bunge la ECOWAS latoa wito wa kufunguliwa kwa mipaka ya Nigeria

    (GMT+08:00) 2019-09-18 09:19:15

    Bunge la Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Magharibi mwa Afrika ECOWAS limesema kufungwa kwa mipaka ya Nigeria na majirani zao wa Afrika hivi karibuni kunaweza kuzuia utekelezaji wa kufanya biashara kwa uhuru katika nchi za jumuiya hiyo. Na kusisitiza kuwa hatua hiyo pia itatoa tishio kwa utekelezaji wa utaratibu wa watu kusafiri kwa uhuru ndani ya kanda hiyo.

    Akihutubia wabunge kwenye kikao cha pili kinachoendelea cha bunge la ECOWAS, Spika wa bunge Moustapha Cisse Lo, amebainisha kuwa hatua hii imekuja wakati Afrika inajitahidi kuongeza juhudi za kuondoa vizuizi kwa ufanisi ndani ya nchi wanachama.

    Mamlaka ya Nigeria imefunga mipaka yake na Benin mwezi mmoja uliopita na kufunga mipaka yake na Niger hivi karibuni, kama hatua ya kukabiliana na changamoto ya magendo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako