• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mjumbe wa China afafanua maendeleo ya nishati ya nyuklia na kazi za kulinda usalama wa kinyuklia nchini China

  (GMT+08:00) 2019-09-18 09:31:23

  Kikao cha 63 cha Shirika la kimataifa la nishati ya atomiki IAEA kilifunguliwa jana Jumanne mjini Vienna. Naibu mkurugenzi wa Idara ya nishati ya atomoki ya China Bw. Zhang Jianhua ambaye ni kiongozi wa ujumbe wa China alihudhuria kikao hicho na kufafanua maendeleo ya sekta ya nishati ya nyuklia na kazi za kulinda usalama wa kinyuklia nchini China.

  Akizungumza kwenye kikao hicho, Bw. Zhang amesema sekta ya nyuklia ya China imedumisha mwelekeo wa maendeleo ya kasi, na kwa ujumla mitambo 47 ya kuzalisha umeme kwa nishati ya nyuklia inafanya kazi na mingine 11 inajengwa sasa.

  Bw. Zhang amesisitiza kuwa, serikali ya China inatilia maanani kazi za kulinda usalama wa kinyuklia. China imedumisha rekodi nzuri ya usalama wa kinyuklia wakati ikisukuma mbele maendeleo endelevu ya sekta hiyo. Amesema kuwa waraka maalumu wa serikali kuhusu Usalama wa kinyuklia wa China uliotolewa kwa mara ya kwanza mapema mwezi huu, umefafanua kwa pande zote kanuni na sera za China za kulinda usalama wa kinyuklia.

  Ofisa huyo pia ametoa wito kwa nchi wanachama wa IAEA kushikilia kanuni ya kushirikiana na kunufaishana, na kujenga kwa pamoja Jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja kuhusu sekta ya nishati ya nyuklia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako