• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Misri yatafuta upatanishi kuhusu bwawa la Ethiopia

  (GMT+08:00) 2019-09-18 09:54:33

  Waziri wa mambo ya nje wa Misri Sameh Shoukry amesema, Misri inakaribisha upatanishi au uingiliaji kutoka chombo chochote kile ambacho kitasaidia kulinda na kufikia maslahi ya nchi zilizoko kwenye Mto Nile.

  Kwenye mkutano na waandishi wa habari akiwa pamoja na mwenzake wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian ambaye yuko ziarani nchini Misri, Shoukry amesema Misri inataka kuisaidia Ethiopia kuzalisha umeme.

  Shoukry amesisitiza kuwa bwawa la GERD la Ethiopia halihitaji ufafanuzi wowote wa kisiasa, na kusema bwawa hilo litachangia kuondoa tofauti zilizopo kwa muda mrefu.

  Ameongeza kuwa wanajaribu kuonesha kuwa kama itakuwepo nia thabiti ya kushughulikia hilo, itahakikisha maslahi ya nchi tatu za Misri, Sudan na Ethiopia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako