• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Russia kufanya juhudi kuongeza mara dufu biashara kati ya pande hizo mbili

    (GMT+08:00) 2019-09-18 19:34:33

    Mkutano wa 24 unaofanyika kila baada ya muda fulani kati ya mawaziri wakuu wa China na Russia ulifanyika jana (tarehe 17) alasiri huko Saint Petersburg, waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang na mwenzake wa Russia Bw. Dmitry Medvedev waliendesha mkutano huo kwa pamoja. Pande mbili zimesema hivi sasa uhusiano kati ya nchi hizo mbili unaendelea vizuri na kuingia kwenye kipindi kipya, inapaswa kuhimiza kuongeza biashara kati yao na kufanya juhudi kutimiza lengo la kuongeza mara dufu biashara kati ya pande hizo mbili.

    Bw. Li Keqiang amesema huu ni mwaka wa 70 tangu uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Russia uanzishwe, hivi karibuni uhusiano huo umeimarishwa zaidi kuwa uhusiano wa wenzi na ushirikiano wa kimkakati kwa pande zote katika zama mpya, na kuimarisha uhusiano huo kunasaidia kulinda ustawi na utulivu wa kikanda na dunia. Alisema,

    "Kutokana na ongezeko la utatahishi wa hali ya kisiasa na kiuchumi duniani, China na Russia ambazo ni nchi jirani na wajumbe wa kudumu kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, zinapenda kuzidisha uhusiano kati yao, kulinda amani ya dunia kwa pamoja na kutafuta manufaa kwa maendeleo ya binadamu. Kufanya hivyo sio tu kutasaidia pande hizi mbili, bali pia kutasaidia dunia nzima, na pande mbalimbali."

    Bw. Li Keqiang amedhihirisha kuwa, China inapenda kuunganisha pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja na jumuiya ya uchumi ya Ulaya na Asia, kuendelea kuhimiza biashara ya pande hizo mbili, kurahisisha zaidi uwekezaji na biashara, na kufanya juhudi katika kutimiza lengo la ongezeko la mara dufu la biashara ya pande hizo mbili.

    Bw. Medevdev amesema kuendeleza uhusiano na China kumepewa kipaumbele na Russia katika sera zake za kidiplomasia, na pia kunalingana na mahitaji ya kujiendeleza ya Russia. Amesema pande hizo mbili zilishirikiana vizuri katika mambo ya kimataifa, na kutetea kuwa kanuni ya kimataifa ya pande mbalimbali inapaswa kutekelezwa, na hatua za upande mmoja zinapaswa kupingwa. Pia amesema Russia inapenda kuzidisha mawasiliano ya kimkakati na ushirikiano halisi na China. Alisema,

    "Baada ya mkutano huu, tutashuhudia pande hizo mbili zikisaini nyaraka karibu 20 muhimu kuhusu ushirikiano kati yao, yakiwemo makubaliano katika sekta ya sayansi na teknolojia, safari ya anga na ya anga ya juu, taarifa ya pamoja iliyosainiwa na wizara ya maendeleo ya uchumi ya Russia na wizara ya biashara ya China kuhusu kupanga ratiba ya maendeleo ya biashara ya bidhaa na biashara ya huduma hadi mwaka 2024, na makubaliano ya ushirikiano kati ya makampuni makubwa ya nchi hizi mbili katika sekta za mafuta, viwanda vya kemikali, malighafi zinazotengenezwa na binadamu, na utengenezaji wa dawa".

    Baada ya mkutano wa siku hiyo, Bw. Li na Bw. Medevdev walisaini taarifa ya pamoja ya mkutano huo.

    Wachambuzi wamesema uhusiano mzuri kati ya China na Russia zote zikiwa nchi wajumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ni muhimu katika kulinda amani, utulivu na ustawi wa dunia.

    Baada ya miaka 70 tangu zianzishe uhusiano wao wa kibalozi, nchi hizo mbili ziko katika kipindi kipya cha mwanzo wa uhusiano wao. China na Russia zitaimarisha kuaminiana kimkakati, kuongeza maslahi yao ya pamoja, kuhimiza maelewano kati ya watu, kulinda utaratibu wa kimataifa ambao kiini chake ni Umoja wa Mataifa na kutoa nguvu kubwa zaidi ya uhai kwenye ushirikiano kati yao. Hii sio tu itasaidia maendeleo ya nchi hizo mbili, bali pia itatoa mchango mpya katika ujenzi wa uhusiano wa kimataifa wa aina mpya, ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja na kulinda amani na utulivu wa dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako