• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika Kusini yaomba msamaha kwa Ghana kufuatia mashambulizi ya chuki dhidi ya wageni

    (GMT+08:00) 2019-09-18 19:34:41

    Waziri wa nchi katika ofisi ya Rais wa Afrika Kusini Bw. Jeffrey Radebe amesema Afrika Kusini imeiomba msamaha Ghana kufuatia mashambulizi ya chuki dhidi ya wageni yaliyotokea nchini humo, na kusababisha vifo na majeruhi ya watu kutoka nchi mbalimbali za Afrika, na biashara zao kuporwa.

    Bw. Radebe amewasilisha maoni ya Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini kwenye mkutano kati yake na Rais Nana Akufo wa Ghana mjini Accra. Pia amesema Rais Ramaphosa ameamua kuahirisha kuhudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa ili kushughulikia jambo hilo.

    Rais Akufo amemshukuru Bw. Radebe kwa kufikisha ujumbe wa Rais Ramaphosa, na kusema anatumai kuwa wahusika wa vurugu hizo watachukuliwa hatua.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako