• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ajali za uzalishaji na vifo kutokana na ajali hizo vyapungua kwa miaka 16 mfululizo nchini China

    (GMT+08:00) 2019-09-18 19:35:56

    Naibu waziri wa usimamizi wa kazi za kukabiliana na hali ya dharura wa China Bw. Sun Huashan, amesema katika miaka 70 iliyopita tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, China imekamilisha kimsingi mfumo wenye umaalumu wa China wa usimamizi wa kazi za kukabiliana na hali ya dharura, na ajali kazini na vifo kutokana na ajali hizo vimepungua kwa miaka 16 mfululizo.

    Bw. Sun Huashan amesema, wakati Jamhuri ya Watu wa China ilipoanzishwa, wastani wa vifo vya watu kutokana na maafa ya asili kwa mwaka ulizidi 7,200, mwaka jana vifo hivyo vimekuwa chini ya watu 1,000, na wakati huohuo ajali kazini na vifo kutokana na ajali hizo vimepungua kwa miaka 16 mfululizo. Bw. Sun anasema,

    "China imeweka sheria zaidi ya 70 zikiwemo sheria ya kukabiliana na matukio ya dharura, sheria ya usalama kazini, na kutoa mipango zaidi ya milioni 5.5 ya kukabiliana na matukio ya dharura. Mfumo wenye umaalumu wa China wa usimamizi wa kazi za kukabiliana na hali ya dharura unakamilika kwa haraka."

    Hivi sasa nyenzo za China za kukabiliana na hali ya dharura haswa ni kikosi cha taifa cha zimamoto na uokoaji, vikosi maalumu mbalimbali vya uokoaji na kukabiliana na matukio ya dharura, na nguvu ya jamii ya kukabiliana na hali ya dharura. Mwaka jana askari laki 1.7 wa zimamoto wa China walitolewa na jeshi, na kuunda kikosi cha taifa cha zimamoto na uokoaji. Naibu mkurugenzi wa idara ya zimamoto na uokoaji ya wizara ya usimamizi wa kazi za kukabiliana na hali ya dharura ya China Bw. Qiong Se, amesema katika karibu mwaka mmoja uliopita, chini ya uongozi wa wizara ya usimamizi wa kazi ya kukabiliana na hali ya dharura, kikosi cha zimamoto na uokoaji kimetekeleza vizuri majukumu yake. Anasema,

    "Majukumu yao yamepanuliwa. Zamani kikosi hicho kilikuwa kinashughulikia ajali za moto tu, na kuokoa maisha ya watu wakati wa matukio ya dharura. Sasa kwa upande mmoja tunashughulikia kukinga matishio makubwa mbalimbali. Na kwa upande mwingine, licha ya moto, pia tunashughulikia ajali nyingine na maafa ya asili, ikiwemo ajali za barabarani, vitu vya kemikali na vitu vingine vyenye hatari, maafa ya mafuriko, ukame, kimbunga, tetemeko na maporomoko ya udongo. Mwaka huu, kazi za kikosi hicho zimeongezeka kwa asilimia 27.9."

    Naibu waziri wa usimamizi wa kazi za kukabiliana na hali ya dharura wa China Bw. Sun amesema, wizara hiyo itaendelea kufuata mawazo ya kuzingatia zaidi maisha ya watu na usalama, na kuimarisha mwamko wa jamii nzima kuhusu umuhimu wa usalama, na pia itaongeza utafiti na matumizi ya teknolojia katika kazi zake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako