• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: Exim Tanzania yazindua kampeni kuhamasisha wateja kuhusu matumizi ya mtiririko wa huduma

  (GMT+08:00) 2019-09-18 19:38:40

  Benki ya Exim Tanzania imezindua kampeni inayolenga kuhamasisha wateja kuhusu matumizi ya mtiririko wa huduma maalumu za kiusalama katika masuala ya fedha zinazotolewa na benki hiyo.

  Mtiririko huo utasaidia wateja kupata huduma mbalimbali ikiwamo ya usafirishaji wa fedha kwa usalama, malipo ya huduma za kisasa za hundi pamoja na huduma ya kuweka fedha kwenye akaunti ya benki hiyo.

  Mkuu wa Idara ya Masoko na Uhusiano wa benki hiyo Stanley Kafu amesema kupitia huduma hizo wateja whawatahitaji kupanga foleni kwenye matawi ya benki hiyo kwa ajili ya kupata huduma za kifedha.

  Akizungumzia huduma ya usafirishaji wa fedha kwa usalama Kafu amesema ina lengo la kumuondolea mteja hatari ya kuibiwa, kuvamiwa, kunyang'anywa fedha wakati wa kuzitoa ofisini kwake kupeleka benki.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako