• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rwanda: Vijana kupata mafunzo kuhusu ujasiriamali wa kilimo

  (GMT+08:00) 2019-09-18 19:39:45

  Vijana 20 kutoka kila wilaya wanaojihusisha na ujasiriamali wa kilimo nchini Rwanda watapata mafunzo kuhusu jinsi ya kuwa na miradi yenye mapato.

  Serikali inapanga kuwatumia vijana hao kutoa mafunzo kwa wenzao kote nchini katika vituo vitakavyoanzishwa katika kila wilaya.

  Rwanda ikiwa na wilaya 30 inamaanisha kuwa viajana 600 watapata mfunzo hayo kwa muda wa miezi 6.

  Vituo hivyo vinaanzishwa chini ya ushirikiano wa chama cha vijana wanalfanya kilimo, vyuo na chuo kikuucha Helsinki nchini Ufini.

  Waziri wa kilimo na mifugo wa Rwanda Dkt. Geraldine Mukeshimana, amesema mpango huo utasaidia kufunguliwa kwa kampuni zaidi kwenye sekta ya kilimo na kuongeza sekta ya kibinafsi nchini humo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako