• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: Tala yafunga ofisi zake Tanzania

  (GMT+08:00) 2019-09-18 19:41:57

  Kampuni ya TALA inayokopesha kwa njia ya mtandao wa simu za kiganjani, imetangaza kufunga shughuli zake Tanzania.

  Imetoa taarifa hiyo Septemba 17, 2019 na kubainisha kuwa maelezo ya kina kuhusu uamuzi huo yatatolewa hivi karibuni.

  Kampuni hiyo inayoendeshwa na teknolojia ambayo kwa sasa inafanya kazi nchini Kenya, Mexico, India na Ufilipino hutoa mikopo ya haraka, na binafsi kwa wakopaji na kuvutia zaidi ya watu milioni 27 duniani.

  Ripoti ya kampuni hiyo mwaka 2018 inaonyesha kuwa katika nchi za Afrika Mashariki asilimia 78 ya mikopo hutumiwa kwa biashara, asilimia 32 ya wateja wake wakiwa wanawake na wanaume, kati yao asilimia 68 wana umri chini ya miaka 34.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako