• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Serikali ya Kenya yatoa pesa kwa serikali za kaunti

    (GMT+08:00) 2019-09-18 19:43:44

    Serikali 47 za kaunti nchini Kenya zitaanza kupokea Sh50 bilioni kutoka Hazina ya Kitaifa kuanzia Ijumaa wiki hii hayo ni kwa mujibu wa kaimu waziri wa Fedha Ukur Yatan.

    Hii ni baada ya Rais Uhuru Kenyatta kutia saini Mswada wa Ugavi wa Mapato (DoRB) wa 2019 Jumanne uliopitishwa baada ya Bunge la Kitaifa na Seneti kukubaliana kuhusu kiasi cha fedha kinachopasa kutengewa serikali za kaunti katika mwaka wa kifedha wa 2019/2020.

    Kulingana na mswada huo, kaunti zimetengewa jumla ya Sh378.1 bilioni, Sh316.5 bilioni zikiwa ni sehemu ya mapato yaliyokusanywa kitaifa huku Sh61.6 zikiwa fedha zilizotengwa mahususi kwa majukumu mahususi katika kaunti.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako