• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • WHO kuisaidia Somalia kuimarisha mfumo wake wa matibabu

  (GMT+08:00) 2019-09-18 20:06:07

  Shirika la Afya Duniani WHO limeahidi kushirikiana na mamlaka za afya nchini Somalia kuimarisha huduma za afya za kimsingi na kuinua uwezo wa wafanyakazi wa matibabu kote nchini humo.

  Mkurugenzi wa WHO katika kanda ya Mediterranean Mashariki Ahmed Al-Mandhari aliyemaliza ziara yake ya kwanza nchini Somalia, amesema WHO itazingatia huduma za afya za kisaikolojia, huduma za matibabu za akina mama na watoto, pamoja na udhibiti wa maradhi ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza. Ametoa wito kwa wafadhili kutambua dhamira ya kisiasa iliyoonyeshwa katika kuhakikisha afya ya wasomali wote na kufanya uwekezaji kwa ajili ya hatma ya Somalia kwa kuzingatia afya ya wasomali.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako