• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Mechi za ligi ya Mabingwa Ulaya-Madrid yaonja muziki wa PSG, Bayern yapeta

  (GMT+08:00) 2019-09-19 08:59:03

  Ligi ya mabingwa Ulaya imeendelea jana kwa michezo kadhaa katika viwanja tofauti, kundi A, Paris Saint Germain imewapiga bila huruma Real Madrid goli 3-0, huku Galatasaray ikilazimishwa sare na Club Bruggle. Kundi B imezikutanisha Olympiacos iliyomaliza kwa sare ya 2-2 na Tottenham Hotspurs, huku Bayern M√ľnchen ikiilaza FK Crvena Zvezda goli 3-0. Na katika kundi C, Dinamo Zagreb imeifurumishia mvua ya magoli 4-0 Atlanta, nayo Shakhtar Donetsk imekubali kichapo cha goli 3-0 toka kwa Manchester City. Michezo ya mwisho ilikuwa ni kundi D, Atletico Madrid imetoshana nguvu ya goli 2-2 na bibi kizee wa Turin Juventus, nao Lokomotiv Moscow ikiimaliza Bayer Leverkusen kwa goli 2-1.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako