• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Aliyekuwa waziri wa Zimababwe asema utaratibu wa ujamaa wenye umaalumu wa China waleta sura mpya kwa China

  (GMT+08:00) 2019-09-19 09:13:32

  Mwanasiasa wa Zimbabwe, ambaye alikuwa waziri wa elimu ya msingi na waziri wa ajira wa Zimbabwe Bibi Fay Chung hivi karibuni alisema kutokana na China kushikilia na kuendeleza utaratibu wa ujamaa wenye umaalumu wa China na kupata njia ya kujiendeleza inayoifaa, China imekuwa na sura mpya ambayo imeonyesha uhai mkubwa wa maendeleo.

  Bibi Fay Chung amesema,

   "Mafanikio yaliyopatikana na China katika miaka 70 iliyopita yanastahili kupongezwa. China siku zote inashikilia utaratibu wa ujamaa, na inaendeleza utaratibu wa ujamaa wenye umaalumu wa China kwa kuendana na mabadiliko ya zama, ili kuhimiza maendeleo ya kijamii."

  Bibi Fay Chung anatumai Zimbabwe itaweza kuiga mfumo wa maendeleo ya China, na kujifunza uzoefu wa maendeleo ya China.

  "hatuwezi kuiga njia ya kujiendeleza ya China moja kwa moja, bali tunapaswa kufuata hali halisi ya Zimbabwe na kujifunza uzoefu wa maendeleo ya China. Kwa hivyo, la muhimu ni kwamba tunapaswa kuweka sera husika ili kukabiliana na changamoto tunazokumbana nazo. Nchini China hakuna mpango unaoweza kutatua masuala yote, na inabadilisha sera zake za kujiendeleza kwa mujibu wa mabadiliko ya hali. "

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako