• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Viwango vya ubora vya FIFA kwa mwezi huu wa Septemba, Tanzania, Burundi, Rwanda zapanda

  (GMT+08:00) 2019-09-20 10:06:21

  Tanzania imechupa kwa nafasi mbili kwenye viwango vya ubora vya shirikisho la mpira wa miguu duniani (FIFA) kwa mwezi huu wa Septemba. Viwango vilivyotangazwa jana Alhamisi na FIFA, Tanzania imepanda kutoka nafasi ya 137 hadi nafasi ya 135 sasa. Rwanda nao wamepanda kwa nafasi tatu kutoka ya 133 hadi 130, Kenya wao wamebakia kwenye nafasi ya 107, Burundi imepanda kwa nafasi nne kutoka nafasi ya 148 hadi nafasi ya 144. Huku Uganda imebakia katika nafasi ya 80 ambayo ilikuwepo pindi viwango hivyo vilipotangazwa mwezi uliopita.

  Ubelgiji bado wanaongoza kwa kuwa nafasi ya kwanza katika ubora wa soka duniani, wakifuatiwa na Ufaransa waliopanda kwa nafasi moja na kuwashusha Brazil, huku Brazil ikikamata nafasi ya tatu, na Uingereza nafasi ya nne, Ureno imepanda kwa nafasi moja na kuwashusha Uruguay ambao sasa wako nafasi ya sita. Uhispania ipo kwenye nafasi ya saba, Croatia nafasi ya nane, Colombia nafasi ya tisa na nafasi ya kumi inashikiliwa na Argentina. San Marino inashikilia mkia ikiwa katika nafasi ya 211.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako