• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Katibu Mkuu UN atoa pongezi maadhimisho ya miaka 70 ya Jamhuri ya Watu wa China

  (GMT+08:00) 2019-09-21 17:34:32

  Ubalozi wa China kwenye Umoja wa Mataifa umefanya tafrija ya kuadhimisha miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya watu wa China. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres, ametoa pongezi zilizosomwa na naibu wake Bibi Amina Mohammed.

  Bw. Guterres amesema China ni mshiriki muhimu wa kazi za Umoja wa Mataifa, na mhimili wa ushirikiano wa kimataifa ambayo ina umuhimu wa kiini. Amesema China na Umoja wa Mataifa zimekuwa zikishirikiana kwenye kukabiliana na masuala yanayoikabili dunia kwa hivi sasa.

  Bw. Guterres amesema China inaongoza kwenye utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu, na imefanya juhudi katika kuondoa umaskini na kuhimiza ushirikiano kati ya Kusini na Kusini. Ameishukuru China kwa kuunga mkono Umoja wa Mataifa katika kukabiliana na changamoto katika sekta ya amani, usalama, haki za binadamu na maendeleo, na ameitakia China ipate mafanikio makubwa zaidi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako