• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa kitabu cheupe kuhusu kazi ya haki za binadamu ya China katika miaka 70 iliyopita

    (GMT+08:00) 2019-09-22 18:29:28

    Ofisi ya habari ya Baraza la serikali ya China leo imetoa kitabu cheupe kuhusu kazi ya ulinzi wa haki za binadamu katika miaka 70 iliyopita toka Jamhuri ya watu wa China kuasisiwa.

    Kitabu hicho kinasema, katika miaka 70 iliyopita watu wa China walijipatia uhuru chini ya uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China. Watu wa China pia wameanza kuwa na utajiri na nguvu zaidi, haki za kimsingi za raia zinaheshimiwa na kulindwa siku hadi siku, pia China inaendelea kutoa mchango katika maendeleo ya mambo ya haki za binadamu duniani.

    Kitabu hicho kimeongeza kwamba, kuwa na maisha bora ni haki kuu ya binadamu. Historia na hali halisi zinaonyesha kuwa katika juhudi za kulinda haki za binadamu, China imefanikiwa kupata njia mwafaka inayoendana na hali halisi ya nchi hiyo na kuustawisha uanuwai wa ustaarabu wa binadamu duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako