• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Juncker asema Umoja wa Ulaya hauwajibiki na matokeo ya Brexit

  (GMT+08:00) 2019-09-23 08:11:33

  Mwenyekiti wa Kamati ya Ulaya Bw. Jean Claude Juncker amesema Umoja wa Ulaya hauwajibiki na matokeo ya Uingereza kujitoa kwenye Umoja huo, na kwamba Umoja huo haupaswi kulaumiwa kwa uamuzi wa Uingereza.

  Akizungumza jana katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Sky News, Juncker amesema Umoja wa Ulaya haujiondoi Uingereza, bali ni Uingereza ndio inajitoa kwenye Umoja wa Ulaya, na kusema Umoja huo hauwajibiki kwa aina yoyote ya matokeo yatakayokuja baada ya Brexit.

  Kauli hiyo imekuja baada ya waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson anaelekea Marekani kuhudhuria mjadala wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, na anatarajiwa kutumia ziara hiyo kuwa na mkutano usio rasmi kuhusu Brexit.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako