Idara ya Ujasusi na Usalama ya Ethiopia NISS imewakamata watu 12 wanaotuhumiwa kupanga mashambulizi ya kigaidi. Kwenye taarifa yake kwa vyombo vya habari, Idara hiyo imesema, watu hao wanatuhumiwa kuwa wanachama wa makundi ya kigaidi ya al-Shabab na IS, na kwamba kiongozi wa kundi la al-Shabab tawi la Ethiopia Mohammed Abdulahi Duilet alikuwa akitafuta maeneo ya kufanya mashambulizi mjini Addis Ababa wakati alipokamatwa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |