• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais Xi atoa salamu za pongezi ya sikukuu ya wakulima kusherehekea mavuno

  (GMT+08:00) 2019-09-23 19:45:10

  Rais Xi Jinping wa China ametoa salamu za pongezi kwa wakulima na watu wanaofanya kazi kwenye sekta ya kilimo na maeneo ya vijijini, wakati China inapoadhimisha siku ya pili ya wakulima kusherehekea mavuno

  Rais Xi ametoa salamu hizo kupitia chaneli mpya ya televisheni ya China CCTV iliyozinduliwa mahsusi kwa ajili ya kilimo na mambo ya kijijini. Rais Xi amesema kukiwa na msingi imara uliojengwa kwa kilimo, China itakuwa na imani kamili ya kuwa na maendeleo.

  Rais Xi amesema mafanikio yaliyopatikana kwenye maeneo yanayohusiana na kilimo, maeneo ya vijijini na wakulima sio tu ni matokeo ya juhudi zote za chama kizima cha kikomunisti, bali pia ni matokeo ya kazi ngumu za wakulima wote na watu wanaofanya kazi kwenye sekta ya kilimo na maeneo ya vijijini.

  Sikukuu ya wakulima kusherehekea mavuno ni siku ya kwanza ya taifa kutengwa mahsusi kwa ajili ya wakulima, ilianza kusherehekewa mwaka jana na itakuwa inaangukia kati ya tarehe 22 na 24 kutegemea kalenda ya kilimo ya China.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako